| Kukamilika kwa ujenzi makao makuu EAC wahitaji Sh7 bil | Send to a friend |
| Friday, 17 June 2011 20:34 |
| 0digg Peter Saramba, Arusha
MATUMIZI ya ofisi za makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), unaotarajiwa kukamilika Agosti mwaka huu, huenda ukakwama kutokana na upungufu wa zaidi ya Sh7.2 bilioni zinazohitajika kukamilisha ujenzi. Mratibu wa ujenzi huo ulioanza mwaka jana, Phil Klerruu, alisema fedha hizo ni ziada ya zile za awali ambazo ni Sh33.6 bilioni, zilizotolewa na Serikali ya Ujerumani ambao ndiyo wadhamini wakuu wa ujenzi huo. Klerruu ambaye ni Maneja Mwandamizi wa Majengo EAC, alikuwa akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo kwa Rais wa zamani wa Ujerumani, Profesa Horst Kohler, alisema fedha hizo zitatumika kujenga uzio wa kisasa kuzunguka ofisi hizo zilizojengwa pembeni mwa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC). “Pia, fedha hizi zitatumika kununua na kufunga vifaa vya kisasa vya mawasiliano (IT equipments), kununua vyombo na vifaa vya kisasa vya jikoni kwa ajili ya mghahawa utakaokuwapo katika ofisi hizi,” alisema Klerruu. wajumbe wa baraza la mashuriano kuhusu nia na hali halisi ya EAC, alisema fedhahizo pia zitatumika kukarabati majengo mawili ya kihistoria yaliyotumiwa na viongozi wa zamani wa jumuiya iliyovunjika mwaka 1977, ili yawe katika mazingira ya kisasa na yaendelee kutumika. Moja kati ya majengo yanayokusudiwa kukarabatiwa, ni lile lililokuwa likitumika kama Ikulu ndogo kabla na baada ya uhuru, ambayo miaka ya karibuni ilikuwa makazi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha kabla ya kukabidhiwa EAC na Serikali ya Tanzania. Ujenzi wa ofisi za EAC umekamilika kwa asilimia 63 kufikia sasa na utakuwa na majengo matatu yenye ghorofa nne, kwa ajili ya ofisi za sekretarieti, Bunge na Mahakama ya Afrika Mashariki. Klerruu aliahidi kuwa watakamilisha mradi huo kwa muda uliopangwa bila gharama za ziada za ujenzi. Profesa Kohler hakutoa ahadi ya moja kwa moja, lakini akasema nchi yake inafuatilia changamoto zinazokabili mradi huo na kwamba, wako tayari kusikiliza maombi rasmi yatakayowasilishwa. |
Add comment
Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!









